Arsenal yaitandika 2-0 Newcastle United

30

Arsenal imeibuka kidedea mbele ya Newcastle United kwa bao 2-0 katika mechi ya Ligi Kuu England mtanange uliopigwa dimba la Emirates Novemba 27 mabao yote yakifungwa kipindi cha pili.

Ukiwa ni mchezo wa kwanza kwa kocha Eddie Howe baada ya ule wa kwanza wa sare ya 3-3 na Brentford kutokuwepo uwanjani kutokana na kuwa muatharika wa virusi vya Covid-19.

Mabao ya Arsenal yamefungwa na Bukayo Saka akitumia vyema pasi ya Nuno Tavares kabla ya Gabriel Martinell kufunga goli muda mfupi baada ya kuingia akitokea bechi akichukua nafasi ya Takehiro Tomiyasu.

Ushindi huo unaifanya Arsenal kurudisha kwenye kuwania nafasi ya nne bora ambapo mchezo uliopita walipigwa na Liverpool bao 4-0 ambapo sasa anashika nafasi ya tano, wakati huo huo Newcastle United wanaalama tano bondeni.

Author: Bruce Amani