Arsenal Yajiweka pagumu, Yatoa Sare na Southampton

34

Vinara wa Ligi Kuu England Arsenal wanaendelea kukutana na ugumu kwenye Ligi kufuatia kutoa sare ya 3-3 na kibonde Southampton mchezo uliochezwa Ijumaa.

Southampton waliweza kufunga magoli mawili ya haraka ndani ya dakika za kipindi cha kwanza kupitia makosa ya kipa Aaron Ramsdale na kuruhusu Xarlos Alcaraz kufunga bao la mapema kisha Theo Walcott akaongeza la pili.

Bao la tatu kwa Southampton likafungwa na Duje Caleta-Car.

Mabao ya Arsenal yamefungwa na winga wa Kibrazil Gabriel Martinelli, nahodha Martin Odegaard na winga wa England Bukayo Saka.

Inakuwa sare ya tatu mfululizo kwa Arsenal ambao wako kileleni kwa tofauti ya pointi tano ya Manchester City ambao Jumatano ijayo watakutana Etihad katika mchezo wa EPL.

Matokeo hayo yanaendelea kudidimiza tumaini la kutwaa kombe la EPL ambapo awali walikuwa kwenye nafasi ya ushindi kabla ya kuanza kutoa sare na kupoteza kwenye mechi hizi za mwishoni wa Ligi.

Southampton wanabakia mwishoni wa msimamo wa Ligi Kuu England ambapo kwenye mechi saba zilizopita wameshindwa kushinda hata mechi moja.

Author: Bruce Amani