Arsenal yakamilisha usajili wa Sambi Lokonga

Arsenal imekamilisha uhamisho wa kiungo kijana wa Ubeligiji aliyekuwa anakipiga kunako klabu ya Anderlecht Albert Sambi Lokonga kwa mkataba wa muda mrefu.

 

Fedha ya uhamisho haijawekwa bayana mpaka sasa lakini inaaminika kuwa ni pauni milioni 17.2.

 

Alijiunga na Anderlecht akiwa na umri wa miaka 15 lakini alianza kucheza mechi ya kwanza mwaka 2017 Disemba ambapo amecheza mechi 78 na kufunga goli 3.

 

“Albert ni mchezaji mzuri sana licha ya umri mdogo lakini amekomaa vyema”, alisema kocha wa Arsenal Mikel Arteta.

 

Arsenal pia inaelekea kukamilisha uhamisho wa beki wa kati wa Brighton Ben White 23, kwa dau la pauni milioni 50, na tayari wamemsajili beki wa kushoto wa Benfica Nuno Tavares, 21, kwa pauni milioni 8.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares