Arsenal yalazimisha Willian kuondoka

Arsenal wanaendelea na mazungumzo ya kusitisha kandarasi ya kufanya kazi ya kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil Willian kabla ya dirisha kubwa la usajili kufungwa.

Endapo uhamisho wa kiungo huyo utashindikana Arsenal itaendelea kulipa fedha kubwa kwa mchezaji ambaye ameshindwa kuonyesha thamani tangia kusajiliwa klabuni hapo akitokea The Blues.

Bado mkataba wa miaka miwili umesalia katika kandarasi ya miaka mitatu ambapo anapokea kiasi cha pauni 200,000 kwa wiki.

Willian, 33, alijiunga na Arsenal kutokea Chelsea kwa mkataba huru, amecheza mechi 25 za Ligi msimu uliopita, msimu huu hajacheza hata mechi moja.

Imeelezwa kuwa mazungumzo ya kusitisha mkataba baina ya wawakilishi wa Willian na klabu kabla dirisha kubwa kufungwa siku ya Jumanne Agosti 31

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares