Arsenal yapeta EPL, yaichapa Everton

Kikosi cha Mikel Arteta kimefanikiwa kupata alama zote tatu kwenye mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Everton kwa goli 3-2 katika mchezo uliokuwa wa piga ni kupige kwa dakika zote 90.

Arsenal ambayo inakamata nafasi ya 9 kwenye msimamo wa EPL ilijikuta iko nyuma kwa goli moja kupitia goli la mapema la Dominic Calvert Lewin ambaye alikuwa anafunga goli la saba chini ya kocha Carlo Anceloti.

Arteta alikuja kunufaika na kiwango bora kutoka kwa Pierre Emerick Aubameyang ambaye alifunga goli mbili katika huo mtanange, goli hizo zinamfanya kufikisha goli 19 msimi huu- jumla akiwa na goli 60 kwenye mechi 95 za Gunners.

Kinda Eddie Nketiah aliirudisha mchezoni Arsenal kwa kumalizia krosi ya kinda mwezake Bukayo Saka na kufanya mchezo kuwa 2-1, kabla Richarlison ajasawazisha dakika chache kabla ya mapumziko.

Ungwe ya pili ilikuwa ya Arsenal ambayo ilifunga goli la tatu na kufanya mchezo kumalizika kwa ushindi wa goli 3-2 huku mwamuzi wa ushindi huo akiwa ni nahodha wa Arsenal Pierre Emerick.

Ushindi huo unaifanya kushika nafasi ya 9 alama mbili kuingia nafasi ya nane, alama tano kukamata nafasi ya tano aliopo United.

Ni mara ya pili sasa Arsenal inashinda michezo miwili mfululizo ya EPL ndani ya msimu huu baada ya kuichapa Newcastle United katikati ya wiki iliyopita na mwanzoni kabisa mwa msimu walishinda mechi mbili mfuatano.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends