Arsenal Yapunguzwa Kasi na Liverpool
Majogoo wa Jiji la Merseyside, Liverpool wameambulia alama moja katika mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya timu ngumu, timu kinara Arsenal mchezo uliopigwa dimba la Anfield.
Ni sare ya bao 2-2 ambapo kocha Jurgen Klopp alilazimika kutokea nyuma na kusawazisha bao hizo.
Mabao ya Liverpool yamefungwa na Mohamed Salah dakika ya 42 na Roberto Firmino dakika ya 87, wakati mabao ya Arsenal ambayo licha ya matokeo hayo inaendelea kuongoza msimamo wa EPL kwa tofauti ya pointi sita yamewekwa kimiani na Wabrazil Gabriel Martinelli dakika ya nane na Gabriel Jesus dakika ya 28.
Kwa matokeo hayo, Arsenal inafikisha pointi 73, ingawa wanaendelea kuongoza Ligi kwa pointi sita zaidi ya mabingwa watetezi, Manchester City ambao hata hivyo wana mechi moja mkononi.
Kwa upande wao, Liverpool wanafikisha pointi 44 katika mchezo wa 29, ingawa wanabaki nafasi ya nane.
