Arsenal yashinda, vita ni Chelsea na Liverpool Kombe la FA

Makinda wa Arsenal wamewatoa kimasomaso mashabiki wa timu hiyo kufuatia kupata ushindi dhidi ya timu ya daraja la kwanza Portsmouth na kujikatia tiketi ya kucheza robo fainali ya Kombe la FA, ushindi unatoa faraja kwa Arsenal iliyotoka kutolewa Europa ligi katikati ya juma lililopita.

Katika mtanange huo kocha Arteta alifanya mabadiliko ya wachezaji sita kulinganisha na kikosi kilichoanza dhidi ya Olympics Ligi ya Europa akawapanga makinda sita wenye umri wa miaka 20 au chini dhidi ya timu ambayo ilikuwa haijapoteza mechi 19 za nyumbani wakishinda 10 mfululizo.

Ushindi wa Arteta ulipitia kwenye goli la mlinzi Sokratis Papastathopouls na Eddie Nketiah ambaye lilikuwa goli la tatu msimu kwa klabu yake ya Arsenal.

Usiku wa leo michezo ya FA itaendelea tena :-

CHELSEA  LIVERPOOL – 22:45

READING  SHEFF UTD – 23:00

WESTBROM  NEWCASTLE UTD – 23:00

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends