Arteta akubali kipigo cha Liverpool 4-0

Kocha wa Arsenal Mikel Arteta amesema walikuwa wanastahili kufungwa na Liverpool kutokana na ubora wa kikosi hicho.

Arteta anasema hayo baada ya kushuhudia kikosi chake kikichapwa bao 4-0 katika dimba la Anfield mchezo uliopigwa Jumamosi huku goli tatu zikifungwa ndani ya dakika 25 pekee ungwe ya pili.

Kipigo ambacho kimehitimisha ushindi wa Arsenal katika mechi 10 mfululizo.

“Wakati tumefungwa goli 1-0 kipindi cha kwanza, tulitakiwa kurudi ungwe ya pili tukiwa makini lakini hatukufanya hivyo,” alisema kocha Mikel Arteta.

“Tumechapwa vizuri sana. Ndiyo maana tumepoteza mchezo”.

Magoli ya Liverpool kwenye mechi hiyo yamefungwa na Sadio Mane, Mohamed Salah, Diogo Jota na Takumi Minamino huku mchezaji nyota akiwa beki wa kulia Trent Alexander Arnold.

Arteta aliongeza kuwa: “Tulijua wanaweza kutufunga. Wanaweza kukaba kwa nguvu, ni moja ya timu bora kwa sasa. Hata hivyo makosa ni sehemu ya mchezo”.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends