Arteta amtumia ujumbe mzuri bosi wake wa zamani Pep Guardiola

366

Kocha wa Arsenal Mikel Arteta ametuma ujumbe kwa bosi wake wa zamani mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola baada ya kushinda Kombe la FA

Mikel Arteta ambaye alikuwa kocha msaidizi wa zamani wa Manchester City alituma ujumbe mzuri kwa Pep Guardiola baada ya kushinda Kombe la FA na Arsenal – kombe lake la kwanza kama meneja.

Pierre-Emerick Aubameyang alifunga mara mbili na kuisaidia Arsenal kukamilisha zamu dhidi ya Chelsea na kushinda 2-1 ugani Wembley.

Guardiola, alimpa meneja huyo wa arsenal kazi yake ya kwanza ya ngazi ya usimamizi, akihudumu kama msaidizi wake katika klabu ya City kwa miaka mitatu.

Arteta aliondoka City kurudi Arsenal kwa jukumu lake la kwanza la usimamizi mwaka jana na kumpiga kwa nguvu bosi wake wa zamani kwenye nusu fainali akiwa njiani kunyakua taji.

Baada ya kushinda tuzo yake kuu ya kwanza, Klabu hiyo imeshinda vikombe 14 vya FA kwa jumla, Arteta alichukua muda wa kushukuru familia yake, pamoja na mshauri wake wa zamani.

“Ninaikosa familia yangu sana wamekuwa kwa njia yote pamoja nami,” Arteta alisema

“Inanimbidi pia kukushukuru Pep kwa njia kubwa sana kwa sababu mimi ni meneja na anenikuza katika hii taluma na leo mimi pia ni meneja kwa hivyo nadhani inabidi pia nizingatie hilo.”

‘Kweli, Guardiola alikuwa mvuto kwangu tangu nilikuwa na miaka 15 na tulikutana huko Barcelona, ​​wote kama wachezaji,’ alisema Arteta.

”Na katika kazi yangu ya ukufunzi na maisha yangu ya kibinafsi, ana ushawishi mkubwa.

‘Ikiwa itanibidi nizungumze juu ya mtu ambaye yeye na maadili yake, njia ambayo amenitendea na jinsi anavyoshughulika na wachezaji na wafanyikazi waliomzunguka, ni jambo la kushangaza.

“Kama mkufunzi, nimejifunza mengi kutoka kwake, tumetumia wakati mzuri pamoja, nyakati nyingine ngumu pia, lakini uzoefu karibu naye umekuwa wa kushangaza.”

Christian Pulisic alikuwa ameipa Chelsea bao safi baada ya dakika tano lakini Aubameyang alitoka kwenye eneo lake baadaye na kufunga bao la mapema kwa njia ya penati kabla ya kuizika Chelsea katika kipindi cha pili.

Ushindi huo una mafanikio kadhaa kutokana na shida ambazo Arsenal wamekuwa nazo msimu huu. Kampeni ya kuenda kucheza Europa imeanza baada ya kuwa gizani, arsenal ilimaliza katika nafasi ya nane katika Ligi Kuu.

Author: John Major Ouma