Arteta asema kucheza fainali yatakuwa mafanikio kwa Arsenal

262

Meneja wa Arsenal Mikel Arteta amesema endapo timu yake itakata tiketi ya kucheza fainali ya Ligi ya Europa kwa kupindua meza mbele ya Villarreal basi yatakuwa mafanikio makubwa kwetu.

Villarreal walishinda bao 2-1 dhidi ya Arsenal mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa nchini Hispania wiki moja iliyopita ambapo winga Nicolas Pepe alikwamisha mpira kwa njia ya penati.

Arsenal watakuwa uwanjani Emirates kumenyana vikali dhidi ya Villarreal Leo Alhamis majira ya saa nne usiku.

“Utakuwa wakati bora sana”, alisema Arteta.

“Sio mimi bali kwa klabu, sio leo bali kwa timu na mashabiki wa klabu hii”.

Arsenal ilitinga fainali ya Ligi ya Europa mwaka 2019 ikiwa chini ya mwalimu wa sasa wa Villarreal Unai Emery, lakini walichapwa bao 4-1 na Chelsea, mchezo uliopigwa Baku.

“Nadhani itakuwa ni hatua kubwa kwetu, itakuwa hatua nzuri kuelekea kwenye mafanikio yetu, tutajaribu hata kushinda tukifika hatua hiyo” alisema Arteta ambaye Arsenal ndiyo timu yake ya kwanza kuifundisha kufuatia kuhudumu kama kocha msaidizi chini ya Pep Guardiola klabuni Man City.

Author: Asifiwe Mbembela