Asensio, Benzema waipa Real Madrid ushindi wa 2-0 dhidi ya Eibar

Strika wa kimataifa wa Ufaransa Karim Benzema ameendelea kuzifumania nyavu kwa kasi baada ya kufunga goli moja katika ushindi wa goli 2-0 walioupata Real Madrid dhidi ya Eibar mchezo wa La Liga uliopigwa Jumamosi hii.

Ushindi huo wa Madrid ambao watakuwa na kibarua kizito siku ya Jumanne kumenyana vikali dhidi ya Liverpool robo fainali ya Ligi ya Mabingwa utawapa nguvu na matumaini ya kufanya vizuri.

Goli la Benzema linakuwa la 24 kwa msimu huu, goli lililofungwa kunako dakika ya 73 ya mchezo, hata hivyo Marco Asensio alifunga mapema bao la kwanza kwa Madrid akimalizia mpira wa Casemiro.

Matokeo hayo yanaifanya Madrid kuwa alama tatu nyuma ya vinara Atletico Madrid kwa alama tatu pekee, ingawa Atleti wana mchezo mmoja mkononi.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares