Asilimia 68 ya wachezaji Ligi ya Kuu Wachanjwa

Uongozi wa Ligi Kuu England umetoa taarifa kuwa takribani asilimia 68 ya wachezaji wanaoshiriki michuano ya Ligi Kuu England wamepata chanjo ya kujikinga na Virusi vya Covid-19.

Taarifa ya Ligi pia imesema wachezaji wengine asilimia 81 walipata chanjo ya haraka, namba ambayo ni kubwa sana kulinganisha na makadirio ya awali.

“Takwimu hizi ni mafuliko kabisa, alisema Prof Jonathan Van-Tam, ambaye ni Naibu Mganga Mkuu.

“Ongezeko la wachezaji na watu wengine kupata chanjo inaonyesha kuwa taarifa imekuwa ikipatikana kwenye vyanzo sahihi, ukipata taarifa kwenye mitandao ya kijamii lazima uwe na shida”.

Hata hivyo, inaaminika kuwa wachezaji wengi zaidi wataendelea kupata chanjo wakiendelea kupata taarifa sahihi.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends