Aston Villa ya Samatta yaendelea kutota, hatarini kushuka daraja

Hofu imeendelea kutanda katika kikosi cha Aston Villa kutokana na hali ya kikosi hicho kwa hivi sasa katika mbio za kukwepa kushuka daraja kufuatia kipigo kutoka kwa Leicester City cha goli 4-0 kipigo ambacho ni cha nne mfululizo cha Ligi na cha tano katika mashindano yote.

Villa ambao wanakamata nafasi ya 19 wamekutwa na kichapo kizito huku Jamie Vardy akiwa amerudi kwa kishindo akifunga goli 2 sawa na Harvey Barnes ambapo sasa Leicester wanaendelea kubakia nafasi ya tatu katika msimamo wa EPL.

Huenda ukawa wakati mgumu kwa Dean Smith kocha wa Aston Villa katika kutafakari namna ya kuinusuru timu hiyo isiangukie katika daraja la timu zitakazoshuka daraja mwishoni mwa msimu huu, ameshafanya usajili wa wachezaji kama Mbwana Samatta, Drink Water na mlinda mlango Pepe Reina.

“Makosa binafsi yamekuwa yakituumiza. Tunahitaji kuwa vizuri zaidi ya hivi tulivyocheza leo. Timu zimekuwa zikiyatumia vyema makosa yetu,” alisema Smith Boss wa Aston Villa.

Tunahitaji kushinda kama hivi kila siku, lakini haiwezekani, tunahitaji kuona tukijiamini karibu na goli, njia pekee ya kupata kujiamini ni kufanya mazoezi kwa nguvu,” alisema Rodgers baada ya mchezo huo.

Author: Bruce Amani

Facebook Comments