Aston Villa yaiduwaza Everton kwa kuilambisha 2 – 0

20

Aston Villa imekusanya alama zote tatu za Ligi Kuu kwa mara ya kwanza tangu timu hiyo ilipopanda daraja kutokea Ligi daraja la kwanza akiifunga Everton goli 2-0.

Mbrazil Wesley na Anwar El Ghazi wamepeleka kipigo cha kwanza kwa Everton msimu huu baada ya kukusanya alama mbili kwenye mechi mbili za awali.

El Ghazi alimalizia pasi sukali ya John McGinn na kumpoteza mlinda mlango John McGinn’s pass.

Matokeo hayo yanaifanya Aston Villa chini ya Dean Smith kuwa katika nafasi ya 11 kwenye msimamo na inakuwa mara ya kwanza kukamata nafasi hiyo tangu 2016.

Licha ya mabadiliko kama kuingia kwa Alex Iwobi na Gomes bado yaliendelea kuwa mabaya kwa Everton ambao wameendelea kuchechemea mwanzoni mwa msimu huu.

Kiujumla makosa binafsi ya wachezaji wa Everton yamepelekea matokeo hayo.

Author: Bruce Amani