Aston Villa yatinga fainali ya Carabao, Samatta alicheza mchezo wa kwanza

Aston Villa imefuzu fainali ya Kombe la Carabao kufuatia ushindi dhidi ya Leicester City wa goli 2-1.

Ushindi wa Aston Villa umepatikana dakika za nyongeza kupitia kwa Trezeguet aliyeingia ngwe ya pili akimalizia pasi ya Mmisri mwezake Ahmed Elmohamady kunako dakika ya 93.

Matokeo hayo yanaifanya Aston Villa kuisubili timu kati ya Manchester City au Manchester United katika mchezo wa fainali utaopigwa dimba la Wembley.

Kikosi cha Dean Smith kinafuzu fainali ya EFL kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2010 kilipofanya hivyo ambapo iliende kupoteza dhidi ya Manchester United mtanange wa fainali.

Katika mchezo wa leo Mtanzania Mbwana Ally Samatta aliyejiunga na Aston Villa dirisha dogo la usajili alianza kikosi cha kwanza ambapo ameonyesha kiwango kizuri licha ya kukosa nafasi mbili za wazi ambazo zingeipa ushindi wa mapema Villa katika mtanange uliopigwa dimba la Villa Park.

Ungwe ya pili Samatta alitolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Devis.

Kesho Jumatano

Manchester City dhidi ya Manchester United mtanange wa awali matokeo ni City 3-1 United

Author: Bruce Amani