Athletic yaichapa Real Madrid sasa kumenyana na Barcelona fainali ya Super Cup

288

Athletic Bilbao watachuana vikali dhidi ya Barcelona mchezo wa fainali ya Super Cup baada ya klabu hiyo kuifunga Real Madrid goli 2-1 mechi ya nusu fainali iliyopigwa Jana Alhamis. Mshambuliaji wa Athletic Bilbao Raul Garcia aliingia kambani mara mbili wakati ambao goli la kufutia machozi kwa Real Madrid likifungwa na strika Karim Benzema.

Athletic watakutana na Barca ambao nao waliifunga Real Sociedad katika hatua ya matuta siku ya Jumatano. Fainali ya Super Cup itapigwa Jumapili Jijini Sevilla.

Author: Asifiwe Mbembela