Atletico Madrid wapigwa 1-0 na AC Milan

Bao pekee la Junior Messias limeipa ushindi AC Milan katika mchezo wa hatua ya makundi uliopigwa dimba la Wanda Metropolitano nchini Hispania dhidi ya wenyeji Atletico Madrid, mtanange uliopigwa Jumatano. Ushindi huo unaifanya AC Milan kufufua matumaini ya kufuzu kucheza hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa ambapo wanasubili mchezo wa mwisho.

Messias mwenye umri wa miaka 30, alitua nchini Italia miaka 10 iliyopita katika klabu ya Crotone na akitokea bechi alifunga goli la kichwa na kutoa maumivu kwa kocha Diego Simeone wa Atletico.

Mechi ya mwisho AC Milan itacheza na Liverpool ambayo tayari imefuzu ambapo ikishinda na Atletico Madrid kusare na Porto watakuwa na uwezo wa kufuzu.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends