Atletico Madrid wapunguza pengo dhidi ya vinara Barcelona

Atletico Madrid imewasogelea vinara wa La Liga Barcelona na mwanya wa pointi mbili baada ya kuwachanbanga Getafe 2 – 0 Jumamosi.

Antoine Griezmann na Saul Niguez waliifungia timu hiyo ya kocha Diego Simeone, wakati Getafe wakipata wakati mgumu baada ya wachezake wake Djene Dakonam na Leandro Cabrera kutimuliwa uwanjani kwa kufanya makosa yaliyosahili adhabu ya kuonyeshwa kadi.

Atletico wamepoteza mara moja tu katika mechi 20 za ligi msimu huu. Sevilla wamesonga juu ya Real Madrid katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi baada ya kuwabomoa Levante mabao 5 – 0. Wissam Ben Yedder, Andre Silva, Franco Vazquez, Pablo Sarabia na Quincy Promes wote waliwafungia wenyeji mabao hao. Barca watacheza na Girona Jumamosi wakati Real wakikabana koo na Espanyol.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends