Atletico Madrid wapunguzwa kasi na Levante kwa kuchapwa 2-0

Vinara wa Ligi Kuu nchini Hispania Atletico Madrid wamepunguzwa kasi ya kuwania taji la Ligi Kuu nchini humo baada ya kukutana na kichapo cha goli 2-0 dhidi ya Levante katika mchezo uliopigwa Leo Jumamosi.

Magoli ya Levante yalifungwa na Jose Luis Morales kunako dakika ya 30 kabla ya Jorge de Frutos’ kuongeza bao la pili dakika za lala salama kabisa.

Kichapo hicho kwa Atletico kinamaanisha kuwa Real Madrid wanaweza kuwasogelea mpaka alama tatu nyuma endapo watashinda mechi yao dhidi ya Real Valladolid itakayopigwa Jumamosi.

Ushindi huo unakuwa wa kwanza wa Levante mbele ya Atletico lakini inakuwa mechi ya kwanza kwa kocha Diego Simeone kupoteza nyumbani tangia Disemba 2019.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares