Atletico Madrid wasogelea taji la La Liga baada ya kuichapa Elche 1-0

Vinara wa Ligi Kuu nchini Hispania La Liga Atletico Madrid wameenda kileleni mwa msimamo wa Ligi kwa tofauti ya alama mbili na timu iliyo nafasi ya pili Real Madrid baada ya kuifunga Elche bao 1-0.

Bao pekee kwenye mechi hiyo limefungwa na Marcos Llorente akimalizia pasi ya winga wa kimataifa wa Ubeligiji Yannick Carrasco kunako dakika ya 23 ya mchezo.

Hata hivyo, Atletico ni bahati pekee iliyokuwa upande wao baada ya Elche kupata tuta dakika za nyongeza ambalo walikosa kupitia kwa Fidel Cjaves licha ya kumuuza mlinda mlango Jan Oblak

Ushindi huo unaifanya Atletico Madrid kufikisha alama 76 huku mechi nne zikiwa zimesalia kumalizika kwa kandanda ya La Liga.

Mechi nyingine iliyopigwa Jumamosi ilikuwa baina ya Real Madrid dhidi ya Osasuna ambayo iliisha kwa faida ya Madrid 2-0.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares