Atletico Madrid waweka rehani ubingwa wa La Liga, wachapwa 1-0 na Sevilla

Vinara wa Ligi Kuu nchini Hispania Atletico Madrid wamekutana na kipigo cha goli 1-0 dhidi ya Sevilla katika mchezo wa La Liga uliopigwa Jumapili.

Bao pekee kwenye mchezo huo limefungwa na Nyota wa Argentina Acuna akimalizia krosi ya beki wa zamani wa Manchester City Jesus Navas na kumshinda mlinda mlango Jan Oblak.

Awali Oblak aliokoa tuta la Lucas Ocampos kufuatia Saul Niguez kumwangusha Ivan Rakitic kwenye eneo la hatari.

Atletico, ambao wanachuchumilia taji la Ligi Kuu kwa mara ya kwanza tangia mwaka 2014 wanaalama tatu juu huku mechi tisa zikisalia.

Barcelona watabakiwa na alama moja pekee kuwakamata vinara Atletico endapo watashinda dhidi ya Real Valladolid Leo Jumatatu.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares