Atletico Madrid yaiadhibu bila huruma Real Madrid

58

Atletico Madrid imeiadhibu bila huruma Real Madrid kwa kuifunga goli 7 – 3 katika mchezo wa kirafiki Ijumaa kujiandaa na msimu wa 2019/20 wa kimashindano unaotegemewa kuanza mwezi Agosti.

Katika ushindi huo mshambuliaji wa Atletico Diego Costa alianza kufunga goli la kwanza katika kunako dakika ya kwanza ya mchezo kabla ya kukamilisha goli tatu kwa maana ya Hat-trick dakika ya 45 ngwe ya kwanza.

Mchezaji ghali wa kikosi cha Atletico Joao Felix, aliyenunuliwa kwa dau la pauni milioni 113 alifunga goli pia katika ushindi wa goli 5-0 kabla ya mapumziko.

Kipindi cha pili Costa alifunga goli 4 kwa upande wake na la 6 kwa upande wa Wabishi Atletico kabla ya kuonyeshwa kadi nyekundu dakika ya 61.

Furaha ya Atletico ilikamilishwa na goli la Vitolo kunako dakika ya 70 na kufanya matokeo kuwa 7-0 kabla Nacho, Karim Benzema na Javier Hernandez kufunga goli la kufutia machozi.

Licha ya Madrid kutumia kiasi kikubwa cha pesa katika usajili wa msimu zaidi ya pauni milioni 300 kutumika bado kocha Zinedeni Zidane ameshidwa kupata muunganiko mzuri wa kikosi chake.

Eden Hazard na Luka Jovic wameshindwa kuingia katika mfumo wa kikosi hicho mapema.

Unakuwa mchezo wa pili kupoteza baada ya kufungwa na Fc Bayern Munich goli 3-1, kisha ikashinda dhidi ya Arsenal kwa penati kufuatia sare ya goli 2-2.

Author: Bruce Amani