Atletico watwaa alama tatu kwa Celta Vigo

222

Mabingwa wa Ligi Kuu nchini Hispania La Liga Atletico Madrid wameibuka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Celta Vigo ingawa timu zote mbili zimemaliza dakika tisini zikiwa pungufu kufuatia kuonyeshwa kadi nyekundu.

Nyota wa kimataifa wa Argentina Angel Correa alifunga goli katika kila kipindi kwa Atletico Madrid lakini kabla ya kufunga goli la pili, Celta Vigo walisawazisha bao la kwanza kupitia kwa Iago Aspas.

Aspas alitumia vyema makosa ya walinzi wa Atletico na mlinda mlango Jan Oblak na kufunga akiwa pembeni mwa lango.

Baada ya hapo wachezaji wawili timu tofauti walionyeshwa kadi nyekundu upande wa Celta Hugo Mallo na upande wa Atletico Mario Hermoso walipewa kwenda kupumzika

Wapinzani wa Jiji moja Real Madrid, walianza vyema kupambana kutwaa ubingwa wa La Liga baada ya kushinda bao 4-1 dhidi ya Alaves Jana Jumamosi.

Barcelona watacheza mechi yao ya kwanza michuano ya Ligi bila huduma ya Lionel Messi aliyeondoka klabuni hapo na kujiunga na Paris St-Germain.

Author: Asifiwe Mbembela