Atletico yailaza Sociedad na kupanda kileleni

59

Atletico Madrid imepanda hadi kileleni mwa La Liga baada ya ushindi mwepesi wa 2-0 dhidi ya Real Sociedad, na kupunguza maumivu ya kichapo cha 4-0 dhidi ya Borussia Dortmund katika Champions League katikati ya wiki.

Beki Diego Godin alifunga bao la kwanza katika kipindi cha kwanza kabla ya beki wa kushoto Mbrzil Filipe Luis kufunga bao la pili na la ushindi katika kipindi cha pili.

Atletico inaongoza na pointi 19 baada ya mechi 10, ijapokuwa mabingwa Barcelona huenda wakapanda kileleni kama watawashinda Real Madrid katika mchuano mkali wa Jumapili maarufu kama “Clasico”, wakati Alaves wanaweza pia kuwaruka Atletico kama watashinda dhidi ya Villarreal

Author: Bruce Amani