Aubameyang arejea na goli Arsenal ikiichapa Newcastle United 2-0

Kikosi cha kocha Mikel Arteta kimepata nguvu mpya kufuatia nahodha wake Pierre-Emerick Aubameyang kurudi kwenye timu baada ya kuwa nje kwa muda mrefu akisumbuliwa na Malaria, kwa kuitandika bao 2-0.

Aubameyang alifunga goli la kwanza baada ya kuwa nje takribani mwezi mzima lakini pia ametoa matumaini kuelekea mtanange wa Alhamis wa mkondo wa pili wa too fainali ya Ligi ya Europa dhidi ya Villarreal huku wakiwa nyuma kutokana na mkondo wa kwanza kuisha kwa 2-1.

Kunako dakika ya 66, kiungo mkabaji raia wa Misri Mohammed Elneny alikwamisha mpira nyavuni.

Akizungumzia juu ya hali yake, Aubameyang amewashukuru madaktari waliokuwa wanahangaikia kadhia yake.

Arsenal, ambao wanacheza Alhamis na Villarreal wanakwea mpaka nafasi ya tisa kwenye msimamo wa Ligi Kuu nchini England.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares