Wageni Mauritania wamekaribishwa vibaya kwenye michuano ya Kimataifa Afrika AFCON baada ya kukubali kipigo kikubwa cha mashindano mpaka sasa cha goli 4-1 dhidi ya Mali katika Kundi E. Timu zote zikiwa zinatokea ukanda wa Afrika Magharibi zilianza mchezo kwa kasi lakini ukosefu wa uzoefu ulionekana changamoto kwa Mauritania kitu kilichowaponza zaidi. Ushindi wa Mali ulipitia
