Ayew atua Al Sadd ya Qatar, anaungana na Xavi Hernandez

Nahodha wa Timu ya Taifa ya Ghana Andre Ayew na mchezaji wa zamani wa Swasea City amejiunga na matajiri wa Qatar, Al Sadd.

 

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 31 anatarajia kutua Mji Mkuu wa Qatar Doha Leo Alhamis Julai 22 kukamilisha uhamisho wake ikiwa ni pamoja na kufanyiwa vipimo vya afya, kabla ya kumwaga wino unaoelezwa kuwa utakuwa ghali.

 

Inatajwa kuwa mchezaji huyo aliyekuwa sehemu ya kikosi cha Ghana kilichofika hatua ya robo fainali ya Kombe la Dunia na kutolewa na Uruguayi ya Luis Suárez atakuwa anapokea kiasi cha dola 200,000 kwa wiki.

 

Ayew atakuwa anafanya kazi chini ya kocha na mchezaji wa zamani wa Barcelona na Hispania Xavi Hernandez ambaye sasa yuko Al Sadd.

 

Ayew alimalizia msimu wa 2020/2021 akiwa kama mfungaji bora wa michuano yote ndani ya klabu hiyo Swansea City akiwa na bao 17 katika mechi 46.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares