Ayub Timbe ajiunga na Reading kwa mkopo

Kklabu ya soka ya Reading nchini Uingereza inayocheza katika daraja la
kwanza, imemsajili Winga wa timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars,
Ayub Timbe Masika, kwa mkopo hadi mwisho wa msimu huu.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27, mzaliwa wa Pumwani jijini
Nairobi, ametokea katika klabu ya  Beijing Renhe ya China ambako
amekuwa akicheza soka tangu mwaka 2017.

Amewahi pia kucheza katika klabu za Anderlecht, Lierse na Genk huko
barani Ulaya.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends