Azam FC Kuikabili Coastal Union ASFC Nusu Fainali

168

Kikosi cha Azam FC kimeanza safari kuelekea Arusha kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Tanzania maarufu kama Azam Sports Federation Cup ambapo watacheza na Coastal Union Mei 29, dimba la Sheikh Amri Abeid.

Azam ambao kwa sasa wanashika nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu baada ya sare ya goli 1-1 na Ruvu Shooting wanategemea wakitwaa taji hilo litawapa upenyo wa kushiriki michuano ya kimataifa msimu ujao.

Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa wapo tayari wa ajili ya mchezo huo na watapambana kupata ushindi.

“Tunakwenda kucheza na wapinzani ambao ni wana timu nzuri na tuna waheshimu kikubwa ni kwenda kutafurta ushindi, mashabiki waweze kuwa pamoja nasi hatutawaangusha.

Mshindi wa Coastal Union na Azam atacheza na mshindi wa mtanange wa Yanga na Simba.

Uwanja huo pia utatumika kwa ajili ya mechi ya fainali katika tarehe itakayotangazwa baadaye.

Author: Asifiwe Mbembela