Azam FC kuwakabili Pyramid ya Misri

Klabu ya Azam FC imeendelea kujiweka sawa kuelekea mtanange mgumu dhidi ya Pyramid FC ya Misri mchezo utakaopigwa dimba la Azam Complex Jijini Dar es Salaam mashindano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.

Kabumbu hilo litapigwa Jumamosi Octoba 16, ambapo kwa mjibu wa taarifa za Azam Fc na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF zimeeleza kuwa mchezo huo utachezwa bila kuwepo kwa mashabiki kutokana na janga la virusi vya Covid-19.

Akizungumzia mchezo huo, Ofisa Habari wa Azam Fc Zakaria Thabit amesema kuwa matarajio makubwa kwa timu hiyo ni kufanya vizuri kwenye kila mchezo ambao watacheza kutokana na uwepo wa wachezaji wazuri pamoja na benchi la ufundi makini.

Hatua ya mchezo huo ni raundi ya pili katika mkondo wa kwanza.

Author: Asifiwe Mbembela

Share With Your Friends