Azam FC yaendelea kuimarisha kikosi 2021/22, yavuta nyota wa Zambia

Azam FC imemtambulisha nyota mpya leo Julai 19 kwa mashabiki wao ikiwa ni mwendelezo wa kuimarisha kikosi hicho kwa ajili ya msimu wa mashindano wa 2021/22.

 

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Zambia, anafahamika kwa jina la Rodgers Kola, mwenye umri wa miaka 32 kwa mjibu wa mtandao wa wikipedia, ni usajili huru akitokea Zanaco ya huko Zambia.

 

Taarifa iliyotolewa na Azam imeeleza kuwa mshambuliaji huyo mzoefu, mrefu na mwenye umbo kubwa, amesaini mkataba mbele ya Ofisa Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin ‘Popat’, utakaomfanya kudumu ndani ya viunga vya Azam Complex hadi mwaka 2023.

 

Kola anakuja kuongeza nguvu kwenye safu ya ya ushambuliaji, kuanzia msimu ujao ambapo awali alikuwa anategemewa zaidi Prince Dube.

 

Aidha, Kola ambaye wakala wake ni Nir Karin, akiwa Zanaco msimu uliopita, alifunga jumla ya goli 14 katika mashindano mbalimbali nchini Zambia.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares