Azam watoa heshima kwa Simba

Licha ya utajiri wao Azam FC Julai 15 wamewapigia makofi mabingwa wa Ligi Kuu Bara 2020/21, Simba katika mchezo wao ambao wamecheza Uwanja wa Azam Complex na kuibuka kwa sare ya bao 1-1.

Azam kutoa heshima kwa Simba ni kutimiza takwa la kisheria ambapo, Kanuni inaeleza kuwa bingwa akipatikana wakati Ligi inaendelea, basi mechi zote ambazo bingwa huyo anacheza atakuwa anapigiwa makofi huku akiwa ametengenezewa gwaride la heshima(guest/guard of honour).
Simba ni mabingwa wa Ligi wakati wakiwa wamebakiza mechi mbili mkononi hivyo katika mechi ya leo Uwanja wa Azam Complex wamepigiwa makofi.
Pointi zao kibindoni ni 80 zimewafanya watangazwe kuwa mabingwa huku Azam FC ikiwa nafasi ya tatu na pointi 65.
Itakabidhiwa taji katika mchezo wa Julai 18 mbele ya Namungo FC, Uwanja wa Mkapa.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares