Azam yabanwa mbavu na Ndanda FC

58

Klabu ya Azam imelazimishwa sare ya goli 1-1 dhidi ya Wanakuchele Ndanda FC katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa dimba la Nangwanda Sijaona Jumatano.

Ndanda ndio waliokuwa wa kwanza kupata goli ngwe ya kwanza kupitia kwa Vitalis Mayanga akitupia bao hilo kunako dakika ya 10.

Ngwe ya kwanza ilimalizika kwa Ndanda kuwa kifua mbele lakini dakika za mwisho za kipindi cha pili zimepelekea mtanange huo kwenda sare ya goli moja kwa moja baada ya Azam kusawazisha goli dakika ya 76 kupitia kwa kinda wa Serengeti boys Andrew Simchimba.

Matokeo hayo yanaifanya Azam kuendelea kukamata nafasi ya pili ya msimamo wa TPL wakiendelea kunufaika pia na udhaifu wa kikosi cha Yanga ambacho kilipata sare kwenye mchezo wao dhidi ya Polisi Tanzania jana Jumanne.

Nahodha wa kikosi cha Ndanda, Kigi Makasi amesema kuwa walikazana kushinda ila bahati haikuwa yao kwani wametawala soka kwa dakika nyingi.

Author: Bruce Amani