Azam yajiunga na Simba, Yanga 16 bora Kombe la ASFC

Azam FC imeibuka na ushindi wa goli 3-1 dhidi ya Friend Rangers katika mchezo wa hatua ya 32 za mwisho kutafuta nafasi ya 16 bora ambapo ushindi huo unaifanya kuungana na vigogo wawili Simba na Yanga katika hatua hiyo sambamba na timu nyingine.

Mabingwa hao watetezi wa Kombe la Shirikisho, wakiwa katika dimba la Uhuru walionyesha kandanda safi ambapo mzani wa kiuchezaji ulionekana ukilemea upande mmoja.

Azam FC walitwaa ubingwa huo kwa kuifunga Lipuli FC bao 1-0 kwenye mchezo wa fainali na bao pekee la ushindi lilifungwa na Obrey Chirwa.Kwa ushindi huo Azam FC Sasa itamenyana na Ihefu ambayo inashiriki Ligi Daraja la Kwanza.

Author: Bruce Amani