Azam yamsajili mshambuliaji wa Ivory Coast

233
Mabingwa watetezi wa Kombe la Kagame Azam FC wamemtambulisha rasmi mshambuliaji wa Kimataifa wa Ivory Coast Daly Ella Richard Djodi kwa ajili ya kuitumikia klabu hiyo kwa msimu wa 2019/2020.
Djodi, 28, ni mchezaji mwenye kimo kizuri akiwa amepita katika klabu mbalimbali tangu kuanza kwake soka la ushindani msimu 2008/2009 akiwa amepita Hire Fc, Stella Club, SOA, Horoya Ac, Leopard.
Kabla ya kujiunga na Azam, Djodi alikuwa anakipiga kunako klabu ya Ashantigold Fc akiwa amefunga goli 17, katika michezo 35, aliyocheza msimu wa 2018/19.
Hata hivyo anakuwa mchezaji wa mwisho kutoka nje ya Tanzania kusajiliwa kwa Wanalambalamba hao kwa msimu huu akiungana na Donald Ngoma, Obrey Chirwa katika safu ya ushambuliaji
Msimu wa 2019/20 Azam itashiriki mashindano ya Kombe la Shirikisho ya Caf, Ligi Kuu Tanzania Bara, FA na Mapinduzi Cup.

Author: Bruce Amani