Azam yamsajili Yvan Lionnel Mballa wa Cameroon

Dirisha kubwa la usajili la Tanzania limefungwa rasmi usiku wa kuamkia Septemba Mosi huku Azam ikimaliza usajili huo kwa usajili nyota wa kimataifa wa Cameroon Yvan Lionnel Mballa.

Usajili wa beki huyo unakamilika kipindi ambacho klabu hiyo imeendelea kujiweka sawa Zambia kwa ajili ya mashindano ya Ligi Kuu, Kombe la Shirikisho Afrika na Kombe la Shirikisho la TFF

Ni dili la mwaka mmoja kasaini beki huyo akitokea Klabu ya Forest Rangers ya Zambia.

Mballa amefunga zoezi la usajili kwenye dirisha lililofungwa usiku wa Agosti 31.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares