Azam yamvuta beki wa Ruvu Shooting Manyama

Mchezaji wa zamani wa Yanga, Namungo na aliyekuwa anakipiga kunako klabu ya Ruvu Shooting Edward Manyama amejiunga na Azam Fc kwa kandarasi ya miaka mitatu.
Beki huyo awali alikuwa anatajwa kumalizana na Simba kwa dili la miaka miwili sasa Azam FC wamepindua meza na kumpa dili la miaka mitatu.

Huu unakuwa ni usajili mkubwa wa kwanza kwa Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina kwa mchezaji mpya mbali na wale ambao wameongezewa kandarasi zao ikiwa ni pamoja na David Bryson, Agrey Morris na Prince Dube.

Azam ambao wanashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara VPL wameanza mapema kujiandaa na msimu ujao wa mashindano ya Ligi na Kombe la FA.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares