Azam yapata ushindi mbele ya Namungo

Azam Fc imevuna alama tatu za kwanza kwenye mechi tatu za Ligi Kuu ya NBC baada ya kuifunga goli 1-0 kikosi cha Namungo Fc mtanange wa uliopigwa dimba la Azam Complex Jijini Dar es Salaam.

Bao pekee kwenye mechi hiyo limefungwa na mshambuliaji kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Idris Mbombo dakika ya 90 akimalizia mpira wa kutengwa (kona) lililompa pointi tatu za kwanza kocha Mzambia, George Lwandamina.
Azam FC inafikisha pointi nne katika mchezo wa tatu, ikitoa sare ya 1-1 na Coastal Union Jijini Tanga kabla ya kuchapwa 2-1 na Polisi Tanzania mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, wakati Namungo FC inabaki na pointi tano kufuatia ushindi wa 2-0 dhidi ya Geita Gold kwenye mechi ya kwanza kabla ya sare ya 1-1 na Kagera Sugar zote Uwanja Ilulu mjini Lindi.

Author: Asifiwe Mbembela

Share With Your Friends