Azam yarudi njia za ushindi kwa kuitandika Mbeya City 2-1 VPL

Azam FC imerejea katika njia za ushindi baada ya kupata matokeo chanya ya goli 2-1 dhidi ya Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu nchini Tanzania mtanange uliopigwa dimba la Azam Complex Jijini Dar es Salaam Jana Alhamis.

Azam mchezo uliopita walipigwa goli 2-1 na Coastal Union ukiwa wa raundi ya pili, wakati wao Mbeya City walilazimishwa sare ya bao 1-1 na mabingwa wa kihistoria wa VPL klabu ya Yanga mchezo uliopigwa Kumbukumbu ya Sokoine Jijini Mbeya.
Magoli ya Azam inayonolewa na kocha George Lwandamina yamefungwa na winga Idd Selemani Nado na mshambuliaji wa kimataifa wa Zimbabwe Prince Dube wakati lile la Mbeya City likiwekwa kimiani na David Mwasa.

Mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Sokoine,  Azam FC ilishinda bao 1-0 na jana ilishinda mabao 2-1 hivyo wamendoka na alama sita jumla mbele ya Mbeya City. Azam FC kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ipo nafasi ya tatu ikiwa imecheza jumla ya 20 na ina pointi 33.

Mbeya City ipo nafasi ya 17 imecheza jumla ya 20 ina pointi 15 kinara wa ligi ni Yanga akiwa na pointi 46 imecheza mechi 20.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares