Baadhi ya matokeo ya ajabu katika historia ya Kariakoo derby

1,171

Yamesalia masaa machache tu kuelekea mtanange uliobeba hisia za wapenzi wa mpira wa miguu Tanzania Yanga dhidi ya Simba, Kariakoo Derby kuchezwa.

Hapa Amani sports News imekuandalia matukio ambayo hayatasahulika kwa haraka.

Yanga 5 – 0 Simba “Sunderland” (Juni 1, 1968).

Huu ulikuwa mchezo uliochezwa wakati bado Simba ikifahamika Sunderland.

Magoli ya Yanga katika mchezo huo yalifungwa na Saleh Zimbwe, na Maulid Dilunga na goli moja alifunga Kitwana Manara “Popat” ulikuwa ni ushindi mkubwa kwa Yanga.

Hiyo ikiwa ni miaka 3 tu tangu ligi kuanzishwa.

Simba v Yanga (Machi 3, 1969)

Mtanange huu una historia kubwa baada ya klabu ya Simba kushindwa kutokea uwanjani na hivyo Yanga kupewa alama 3.

Mchezo huu ulikuwa unaenda kuchezwa miezi kadhaa baada ya Simba kufungwa goli 5, hivyo kushindwa kufika uwanjani ilihusishwa na kuogopa kupoteza kwa idadi kubwa tena ya magoli.

Simba 6 – 0 Yanga (Julai 19, 1977)

Huu ni mchezo ambao umeendelea kuziganda rekodi zake, moja ni idadi kubwa ya magoli, pili katika mchezo huo Abdallah Athumani Seif Kibadeni “King” alifunga goli 3 katika mtanange huo.

Rekodi hiyo inashikiliwa mpaka sasa, hakuna mchezaji mwingine ambaye amewai kufunga goli tatu katika mchezo mmoja wa Kariakoo Derby dhidi yake.

Kibadeni alifunga goli dakika ya 10, 42, na 89, magoli mengine yalifungwa na Seleman Sanga goli la kujifunga (OG) na Ezekiel Greyson

Simba ilifanikiwa kuubeba ubingwa msimu huo mbele ya Yanga ambayo ilikuwa ikikumbwa na matatizo ya ndani ya timu kama ilivyo sasa.

Yanga 0 – 5 Simba (Mei 7, 2012)

Huo ni ushindi zaidi mkubwa mpaka sasa 2019.

Staa wa Uganda Emmanuel Okwi alikuwa katika kiwango bora sana katika mtanange huo ambapo alifunga goli 2, Juma Kaseja, Felix Sunzu, na marehemu Patrick Magisango walikuwa wafungaji katika derby hiyo.

Mchezo huo ulikuwa wa mwisho kuchezwa wakati Simba tayari imetwaa ubingwa wa Ligi kuu Tanzania bara mpaka sasa haijawai kutokea.

Simba 3 – 3 Yanga (Oktoba 20, 2013).

Iliwachukua dakika 45 tu Yanga kufunga goli 3 katika mtanange ambao ulionekana kama umeinama upande mmoja baada ya goli la Mrisho Ngassa na Hamis Kiiza kufunga mawili.

Kipindi cha pili kilikuwa tofauti jambo lililoisaidia zaidi Simba ambapo ilifanikiwa kurudisha magoli yote kupitia kwa Bertram Mwombeki, George Owino na Gilbert Kaze.

Kuamka na kupambana kuliisaidia Simba kutoka nyuma goli 3 na kutoka sare ya goli 3-3. Kuna michezo mingi ambayo ina historia zinapokutana timu hizi nyingine zikiwa zinatazama waamuzi na wengine mashabiki.

Kwa takwimu zilitolewa mwaka 2017 inaonyesha hii ni derby tano kwa ubora Afrika, kwa upande wa Afrika Mashariki inaendelea kushika nafasi ya kwanza.

Author: Asifiwe Mbembela