Baba wa Champions League Johansson afariki dunia

Lennart Johansson , rais  wa  zamani  wa shirikishio la  kandanda  barani  Ulaya  UEFA  anayeangaliwa  kama  baba  wa  mashindano  ya  Champions League  katika  bara  hilo, amefariki dunia akiwa  na  umri  wa  miaka 89, shirikisho  la  kandanda  nchini  Sweden  limesema leo Jumatano. “Soka  nchini  Sweden  linaomboleza,” shirikisho  la  soka  nchini  humo  limesema.

Kipindi  cha  uongozi  wa  Johansson  katika  shirikisho  la  kandanda  barani  Ulaya  UEFA, kuanzia  mwaka  1990  hadi  2007, uliingiliana  na  kuzaliwa  kwa  Champions League, mashindano  makubwa  kabisa  duniani  ya  vilabu, na mabadiliko  makubwa  ya  kandanda  kuwa  biashara  kubwa  dunia kwa  kuwa  na  mvuto  mkubwa  na  mapato yaliyoelekezwa  na  mapato  kutokana  na  televisheni.

Tangazo  la  kifo  chake  Johansson , akiwa  kipenzi cha  wengi  licha  ya  sifa  yake  ya  mtu  asiyependa  mchezo, limekuja  muda  mfupi tu kabla  ya  ufunguzi wa  mkutano  mkuu  wa  FIFA  mjini  Paris  ambako  wajumbe  ikiwa  ni  pamoja  na  rais Gianni Infantino walikaa  kimya  kwa  muda  wa  dakika  moja  kumkumbuka.

“Nimevunjika  moyo kutokana  na  taarifa  hizi  za  kuondokewa  na  Lennart Johansson,” Infantino  amesema  taarifa. alikuwa  raifiki  na kisima  cha  hekima  kubwa  na hamasa. Nitamshukuru  milele  kwa  kuwa  nae  akiwa  rais  wa  UEFA  wakati  ninajiunga  na  shirikisho  hilo  mwaka  2000.

Alizaliwa  Novemba  5, 1929 katika  familia  ya  kawaida  mjini  Stockholm katika  kitongoji cha  Bromma, Johansson alipanda ngazi  kuanzia  akiwa mhudumu  kwa  mkurugenzi wa  kampuni  ya  ujenzi. Alianza kuwa  kiongozi wa  masuala  ya  mpira  wa  miguu  katika  miaka  ya  1960, akiwa  rais wa  klabu  kubwa  ya  Sweden ya  AIK, na  kisha  kuwa  mkuu  wa  shirikisho  la  kandanda  la  Sweden  kabla  ya  kuchaguliwa  kuwa  mkuu  wa  UEFA mwaka  1990.

Author: Bruce Amani