Bakayoko apelekwa AC Milan mkopo

Kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa Tiemoue Bakayoko amejiunga na AC Milan kwa mkataba wa miaka miwili wa mkopo akitokea Chelsea ya England.

Bakayoko, 23, anarejea klabuni hapo kufuatia msimu wa mwaka 2018/19 kutumika viunga vya San Siro akiendelea kukosa nafasi ya kuanza kwenye kikosi cha The Blues.

Bakayoko akiwa kwenye msimu wake wa kwanza alicheza jumla ya mechi 43 baada ya kusajiliwa kutokea Monaco kwa dau la pauni milioni 40 mnamo mwaka 2017.

Kushindwa kufikia kiwango tarajiwa kinamfanya mchezaji huyo kuendelea kutanga tanga sehemu ya kucheza tangia kuhamia Chelsea.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares