Balotelli aweka rekodi ya kuonyeshwa kadi nyekundu

58

Mario Balotelli, 29,  ameweka rekodi ya aina yake baada ya kuwa mchezaji wa pili kwa kuonyeshwa kadi nyekundu nyingi zaidi baada ya Jemerson wa Monaco ambaye yeye (Balotelli) ana kadi 13.

Akitokea bechi, Super Mario alitumia dakika saba pekee kuandika rekodi hiyo akiwa ameonyeshwa kadi ya njano kufuatia na nyekundu kwenye mchezo wa Serie A dhidi ya Cagliari, mtanange ulioisha kwa sare ya goli 2-2.

Strika huyo wa Brescia hana msimu mzuri klabuni halo tangu msimu huu kuanza mwezi Agosti amefunga goli tano pekee ambapo kadi hiyo inamfanya kukosa mchezo wa Ijumaa dhidi ya AC Milan.

Kadi ya leo inakuwa ya 13 na kuwa mchezaji wa pili katika ligi tano bora kuonyeshwa kadi nyekundu nyingi pembeni ya mlinzi wa Monaco Jemerson.

Wiki iliyopita Rais wa Brescia alisema Balotelli yupo huru kwenda popote katika dirisha dogo la Januari kwani hana msaada kwa timu inayopambana kukwepa kushuka daraja.

Brescia wanakamata nafasi ya 18 alama moja kutoka kwenye mstari wa kushuka daraja.

Author: Bruce Amani