Balozi wa Tanzania Nigeria aongeza mzuka Simba dhidi ya Plateau United

220

Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Dkt Benson Bana amewapa motisha wachezaji wa Simba kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa barani Afrika utakaopigwa dimba la Jos Novemba 29, baada ya kuwatembelea kambini waliko wachezaji na viongozi na kasha kuongea nao.

Akizungumza na wachezaji hao balozi huyo amesema “Kila kitu kipo sawa na ushirikiano umekuwa mkubwa hapa Nigeria hivyo tunaamini kwamba safari ya kwenda mjini Jos itakwenda vizuri na mtakuwa salama pia,” amesema.

Wakati hali ikiongezeka kwenye kikosi cha Simba kilicho chini ya Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck leo kinaondoka Lagos ambapo kiliweka kambi kwa muda kuifuata Plateau United katika mji wenye makao makuu ya klabu hiyo.

Mchezo huo utachezwa kwenye Uwanja wa New Jos wenye uwezo wa kuchukua watu 40,000, majira ya saa 12 jioni masaa ya Afrika Mashariki na Kati. Balozi wa Tanzania nchini Nigeria, Dk Benson Bana amekuwa kati ya watu waliotilia mkazo suala hilo la kutumia usafiri wa ndege. Balozi huyo amesema kuwa anaamini timu hiyo itafanya vizuri na kikubwa ambacho kinahitajika ni ushindi katika mchezo huo.

Author: Asifiwe Mbembela