Bao la Ajib laongeza utamu ushindi wa Yanga

18

Achana na matokeo ya ushindi wa magoli 2 – 0 waliopata Mabingwa wa Kihistoria wa ligi kuu ya Tanzania Young Africans dhidi ya Mbao FC Jumapilisi usiku tarehe 07 0ktoba 2018 katika uwanja wa taifa Dar es Salaam na kuipeleka timu hiyo katika nafasi ya pili ya msimamo wa ligi hiyo

Stori kubwa katika mchezo huo ni goli la dakika 90 lililofungwa na mchezaji Ibrahim Ajib Migomba “Ibracadabra” kwa style ya “Acrobatic” na kuamsha nderemo kwa mashabiki wa soka huku wakieleza kuwa ni moja kati ya goli bora kufungwa katika ligi hii,

Wakiwa kifua mbele kwa goli moja lililofungwa na mchezaji Rafael Daud Lotti katika kipindi cha kwanza vijana wa Mbao FC waliwasakama Yanga kwa muda mwingi wa mchezo kitu ambacho kilizua hofu kwa mashabiki wa timu hiyo kuona huenda vijana hao wa Mbao FC wanaweza kukomboa goli hilo na kufanya Yanga isiibuke na ushindi katika mchezo huo

Mwamuzi wa mpambano huo aliongeza dakika tano kufidia dakika zilizocheleweshwa huku Mbao wakiwa wanashambulia kwa nguvu goli la Yanga, ilipigwa Counter Attack goli kwa Mbao FC, krosi ya mchezaji Gadiel Michael ilishindwa kuokolewa vilivyo na beki wa Mbao FC mpira huo ulimfikia Ajib na kupiga acrobatic na mpira kugonga ‘BESELA na ‘baadae kugonga chini kwenye mstari na kuingia ndani ya nyavu na kuandika goli la pili na kuamsha nderemo na vifijo  kwa vijana hao wa jangwani.

Mashabiki wengi wamelifananisha goli hilo na la wachezaji wakubwa barani Ulaya kama goli la Cristiano Ronaldo alilofunga wakati akiwa Real Madrid dhidi ya Juventus katika mchezo wa robo fainali ya ligi ya Mabingwa Barani Ulaya wengine wakisema kama la mchezaji Gareth Bale alilofunga dhidi ya Liverpool katika fainali ya Uefa Champions League huku wengine wakisema aliwahi kufunga mchezaji Wayne Rooney katika mchezo kati ya Manchester United dhidi ya Manchester City.

Kwa ushindi huo, Yanga SC inafikisha pointi 16 baada ya kucheza mechi sita, sawa na Singida United yenye wastani mdogo wa mabao na mechi tatu zaidi za kucheza – wakizidiwa pointi moja na Mtibwa Sugar wanaoongoza Ligi Kuu kwa pointi zao 17 za mechi tisa.

Mabingwa watetezi, Simba SC wao wapo nafasi ya nne kwa pointi zao 14 baada ya kucheza mechi saba, wakizidiwa pointi moja na Azam FC iliyocheza mechi saba pia.

Matokeo mengine ya ligi kuu kwa michezo iliyopigwa Jumapili Oktoba 07 2018 ni  Maafande wa JKT Tanzania wamelazimishwa sare ya goli 1- 1 dhidi ya Alliance huku Biashara United ya Mara ikilala nyumbani kwa magoli 0-2 dhidi ya Mwadui FC, na huu ni ushindi wa kwanza kwa timu hiyo ya Mwadui toka mkoani Shinyanga kwa msimu huu wa 2018-19

Author: Bruce Amani