Bao la Messi lawapa Barcelona taji la 26 la ligi ya Uhispania

Barcelona wamebeba taji lao la 26 la La Liga baada ya kupata ushindi wa 1 – 0 dhidi ya Levante shukrani kwa bao la kipindi cha pili kutoka kwa Lionel Messi aliyeingia uwanjani kama mchezaji wa akiba. Barcelona sasa wameshinda mataji 8 ya La Liga katika misimu 11.

Huku wakisubiri mechi ya mkondo wa kwanza wa nusu fainali ya Champions League Jumatano dhidi ya Liverpool, Messi hakuanza mechi hii.

Baada ya kipindi cha kwanza kukamilika kwa sare tasa, Muargentina huyo aliingia uwanjani na kubadilisha mambo alipochukua pasi ya kichwa ya Arturo Vidal na kuwachenga mabeki wa wawili wa Levante na kusukuma mpira wavuni

Barca wanawinda mataji matatu katika msimu huu, Ligi kuu ambayo wamechukua, Champions League na Copa del Rey.

Watacheza fainali ya Copa del Rey dhidi ya Valencia Mei 25

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends