Barca kupepetana vikali na Atletico Madrid katika vita ya ubingwa La Liga

438

Barcelona watakuwa nyumbani kuwakaribisha vinara Atletico Madrid Jumamosi katika miongoni mwa michezo muhimu ya kusaka nafasi ya ubingwa wa Ligi Kuu nchini Hispania La Liga.

Kabla ya mchezo huo, mwezi Januari Atletico walikuwa kileleni kwa tofauti ya alama 13 lakini Barcelona wamefuta pengo hilo mpaka moja ambapo ushindi kwenye mechi hiyo utaipandisha nafasi ya kwanza ikiwa ni mara ya kwanza kwa msimu huu.

Real Madrid, wako nafasi ya pili kwenye msimamo wa La Liga zikiwa sawa alama na Barca, na watachuana vikali dhidi Sevilla siku ya Jumapili.

Hata hivyo, kocha Zinedine Zidane Ana faida endapo watafanana kialama na Barcelona kutokana na kushinda mechi iliyowakutanisha baina yao.

Kocha wa Barcelona Ronald Koeman kwenye mechi ya Kesho Jumamosi, atakuwa jukwaani anamalizia adhabu yake ya matumizi ya mabaya ya maneno.

Author: Bruce Amani