Barca yapepea kileleni licha ya Dembele kuumia

45

Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi akitokea bechi imeisaidia klabu hiyo kupata ushindi wa goli 3-1 dhidi ya Leganes na kuendelea kujiimarisha kileleni kwa alama 5 zaidi kunako La Liga.

Kocha Ernesto Valverde alimpumzisha staa wake Messi ingawa kiwango bora cha Ousmane Dembele kilimfanya atabasamu mapema baada ya kuitanguliza klabu hiyo kabla ya Martin Braithwaite kusawazisha katika dakika ya 32 ya mchezo.

Shuti kali la Messi lilipanguliwa na Mlinda mlango Ivan Cuellar kabla ya Luis Suarez kumalizia mpira huo na kuiandikia goli la pili kwa Wakatulanya hao.

Muajentina huyo alifunga goli lake katika dakika za mwishoni baada ya kazi murua ya Jordi Alba na kuendelea na rekodi nzuri katika ligi kuu nchini Hispania.

Matokeo hayo yameifanya Fc Barcelona kufikisha michezo 7 bila kupoteza katika ligi, ingawa staa wao Dembele hakumaliza mchezo huo baada ya kutolewa nje ya uwanja dakika ya 68 akisumbuliwa na majeruhi ya enka huku akionyesha kiwango bora sana tangu amesajiliwa akitokea Borrusia Dotmund mwaka 2017.

Author: Bruce Amani