Barca yapoteza 1-0 kwa Bilbao Copa del Rey

Majanga yamezidi kuiandama Barcelona baada ya hapo jana usiku kuadhibiwa na Athletic Bilbao goli 1-0 na kuondolewa rasmi katika michuano ya Copa del Rey hatua ya robo fainali kipigo kinacho maanisha ndoto za kufuzu mara saba mfululizo michuano ya Rey zimeishia ukingoni.

Katika mtanange uliokuwa wa piga ni kupige licha ya Barca kutawala kwa kiasi kikubwa, Bilbao walihitaji kusubili mpaka dakika tatu za nyongeza kuiangamiza Barcelona ambayo majanga yameendelea kuiandama kwa za hivi karibuni.

Goli pekee katika mchezo huo lilitiwa kimiani na Inaki Williams kwa kichwa mpira uliomshinda mlinda mlango Marc-Andre ter Stegen.

Ikumbukwe Barcelona ilikuwa katika mgogoro baina ya Mkurugenzi wa michezo Abidal na Lionel Messi mwanzoni mwa wiki hii lakini viongozi wa juu wakasuluhisha na kumaliza tofauti zao, matokeo ya leo bila shaka yataendelea kuichanganya zaidi Barca.

Kipigo cha Barcelona kinaandikisha historia ya kutoshuhudia timu kubwa za Real Madrid na Barcelona hatua ya fainali ya Copa del Rey tangu mwaka 2010 ilipotokea hivyo.

Matokeo mengine Mirandes iliichapa Villarreal 4-2 wakati Granada ikishinda dhidi ya Valencia 2-1 na kuingia nusu fainali ya michuano hiyo

Author: Bruce Amani

Facebook Comments