Barca yarejea kileleni mwa La Liga kwa kishindo

Lionel Messi alifunga mabao mawili kupitia mikwaju ya freekick wakati Barcelona ilishinda derby ya Catalan kwa kuinyoa Espanyol 4-0 Jumamosi. Ilikuwa mara ya kwanza kwa Messi kufunga mabao ya freekick za moja kwa moja katika mchuano mmoja wa La Liga.

Luis Suarez na Ousmane Dembele pia walibusu nyavu wakati Barca wakijiimarisha kileleni mwa ligi kuu ya Hispania kwa pengo la pointi tatu.

Awali, Atletico Madrid iliifunga Alaves 3-0 katika dimba la Wanda Metropolitano na kufikisha pointi sana na nambari mbili Sevilla ambao walitoka sare ya 1-1 na Valencia. Nikola Kalinic aliiweka Atleti kifua mbele kunako dakika za 25 kwa kuunganisha krosi ya Arias, ikiwa ndio bao lake la kwanza la ligi kwa klabu hiyo. Antoine Griezmann alifunga bao la pili katika dakika ya 82, kabla ya Rodrigo Hernandez kumaliza kazi zikiwa zimesalia dakika tazu mchezo kukamilika.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends